Terror Suspect Released
Hawa Mohammed aliyetiwa nguvuni na kikosi cha maafisa wa kupambana na ugaidi nchini kwa tuhuma za kuhusika na shambulizi la kigaidi lililowaua watu 76 nchini uganda mwezi wa saba , hatimaye ameachioliwa huru. Kwa mujibu wa afisa mkuu wa polisi wa Pwani ya Kenya leo Nyongesa, hawa aliachiliwa huru baada ya kuhojiwa na kupatikana hana makosa yoyote yanayoweza kumhusisha na mashambulizi hayo. Alitiwa nguvuni hapo jana katika mtaa wa Majengo, siku mbili tu baada ya mumewe Habib Suleiman aliye mtangazaji wa kituo cha radio salaam kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi hayo ya kigaidi. Suleiman anahojiwa na maafisa wa ujasusi na haijabainika ikiwa atasafirishwa hadi nchini Uganda au la.
--------
The wife of a Mombasa based Radio journalist  arrested by anti terrorist police unit has been released. According to area police boss Leo Nyongesa  , Ms Hawa Mohammed was found innocent after interrogations.